MAANA HALISI YA MWEZI WA 12 {DECEMBER}

| Makala

DECEMBER KIROHO:

Mara kadhaa tumekuwa tunachukulia mwisho wa mwaka {december} kama mwezi wa mapumziko na kibaya zaidi huwa watu hawapumziki kimwili tu, wanapumzika mpaka kiroho kabisa.
Wengi wanakuwa hawana ratiba tena za maombi na mifungo zaidi kwa sababu ni kama wameshafunga na kuomba sana,sasa wanatafuta nafasi ya mapumziko kwa ajili ya kuusubiri mwaka mpya uingie ndipo waanze ratiba za kiroho.

Ukweli ni huu, December ama mwisho wa mwaka ni muda wa kiroho zaidi ambao unapaswa kuutumia kiroho ili kuhakikisha unajipanga kwa majira mapya na msimu mpya wa mwaka mpya.
Kwa kawaida iko hivi mtu wa Mungu, december ni mwezi wa ku set mipango yako kiroho zaidi katika kuukabili mwaka mpya unaokuja.


2026 unayoitarajia, inaandaliwa muda huu december 2025.
Na ikitokea umefeli kujipanga kwenye december kwa ajili ya mwaka mpya, ukweli ni kwamba mwaka wako unaweza kuwa mzito sana na utajitutumua sana katika kuzipata ahadi za Mungu kwenyte maisha yako.

Nikusaidie kitu hapa, December ni LANGO, na ni lango la mwaka mpya….
December haifungi tu mwaka, inaufungua pia mwaka mpya. Ukikosea kukaa mguu sawa kiroho december imekula kwako.

Adui anatambua kuwa december ni mlango wa kuingia majira mapya na ndio maana huwa anapambana kuhakikisha anatimiza mipango yake mitatu ndani ya watu wa Mungu, mipango yake kama ilivyoandikwa katika kitabu cha Yohana 10:10a “mwivi haji ila aibe na kuchinja na kuharibu”
Ndio maana utasikia sana vifo vinatokea mahali mahali kama vinavyosababishwa na ajali mbalimbali,magonjwa nk.
Hii ni kwasababu adui hataki uvuke mwaka uingie kwenye majira mapya ya kutembea katika ahadi za Mungu wako.


Hakikisha unakuwa mwaminifu sana kufuatilia mafundisho hapa madhabahuni ili yakusaidie kuona namna ambavyo unaweza kuitumia december kiroho kwa ajili ya kumiliki ahadi za Mungu kwa mwaka mpya unaokuja {2026}


Kitabu cha Hesabu 13:1-33 kinaeleza kwa habari za wapelelezi ambao walitumwa na Musa ili kuipepeleza nchi waliyoahidiwa na Bwana Mungu kuwa atawapa baada ya kuwatoa utumwani Misri.

PATA MUDA USOME SURA NZIMA YA 13 YA KITABU CHA HESABU, tutaanzia hapo kujifunza kuhusu December kiroho.

NB: IBADA LIVE KILA SIKU USIKU SAA SITA {Youtube SIRI ZA BIBLIA}

Namba ya msaada wa kiroho madhabahuni,maombi na maombezi +255 758 708804

Pastor Innocent Mashauri
Madhabahu ya SIRI ZA BIBLIA
Maarifa ya ki-Mungu


 SADAKA